Na A.H.Hamad
Mratibu Mkaazi
wa Umoja wa Mataifa Tanzania Alvaro Rodriguez amesema afisi yake inafanya kazi
kwa karibu sana na mamlaka za serikali na taasisi za kiraia kuhakikisha kuwa
Uchaguzi mkuu ujao unafanyika kwa umakini, uwazi na kwa amani.
Akijibu masuali
ya waandishi wa habari katika mkutano na Wanahabari wa Zanzibar uliafanyika
katika ukumbi wa afisi ndogo ya UN Zanzibar Bw. Rodriguez amesema ijapokuwa UN
haina nguvu za kutosha kuhakikisha kuwa kila kitu kinaenda sawa lakini
inafahamu kuwa inalojukumu la kuhakikisha kuwa inashirikiana na vyombo husika
ili kupunguza joto la uchaguzi na kuhakikisha haki za watu wote zikiwemo za
watoto, wanawake na walemavu zinaheshimiwa na kulindwa kabla, wakati na baada
ya uchaguzi.
Ametaja baadhi
ya hatua zinazochukuliwa na UN katika kufanikisha hilo kuwa ni pamoja na
utekelezaji wa Mradi wa miaka mitatu wa
Ujengaji Uwezo wa Demokrasia (Democratic Empowerment Project) ambao
pamoja na mambo mengine unasaidia kuimarisha uwezo wa Tume ya uchaguzi Zanzibar
na wadau mbali mbali wa uchaguzi wa uchaguzi ili dhamira ya kuhakikisha Amani
iliopo inaendelea kudumu inafanikiwa.
Hata hivyo
mratibu huyo mkaazi aliwakumbusha wanahabari kuwa pamoja na machango huo wa UN
wanahabari nao wanajukumu kubwa la kuhakikisha uchaguzi wa Amani hasa kwa
kuzingatia ushawishi wa yale wanayoyaandika, kuyatangaza na kuyapiga picha kwa
wananchi wanaowafuatilia.” Himizeni Amani, toeni habari sahihi na shawishini
mijadala/mazungumzo miongononi mwa wadau mtakuwa mmesaidia” alisema.
Akitoa ufafanuzi
wa mchango wa Umoja wa Mataifa katika mradi huo wa ujengaji uwezo wa Demokrasia
Msimamizi wa Mradi Bi Hamida Kibwana amesema Umoja wa Mataifa umeisaidia tume
ya Uchaguzi kupata vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi na kuwakutanisha wadau wa
uchaguzi na vijana katika majadala ya kisiasa ili kujenga mazingirira ya
kuelewana na kukuaminiana kabla wakati na baada ya uchagu.
Sambamba na hayo
mradi utajumuisha pia mafunzo kwa wanahabari ili waweze kuandika vyema habari
za uchaguzi na kuwapatia pia mafunzo maafisa wa polisi juu ya njia bora ya
kukabiliana na rabsha za uchaguzi bila kutumia nguvu nyingi na kwa njia ambayo
inaheshimu haki za binaadamu.
Amesema mradi
huo umesaidi pia kutayarisha maadili ya uchaguzi kwa Vyama vya siasa ambayo yalitiwa
saini hivi karibuni Zanzibar na tayari maafisa wake wamepata fursa ya kujifunza
utaratibu uliotumiwa na Kenya katika kuratibu matokeo ya uchaguzi ili yasilete
mkanganyiko kwa wananchi na kuwa chanzo cha vurugu.
Nae Mkuu wa
Afisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar Anna Senga amesema Umoja wa mataifa unania ya dhati ya
kuimarisha demokrasia Zanzibar na ndio maana pamoja na misaada mbali mbali
inayotolewa katika kuhakikisha uchaguzi wa Amani imekuwa pia ikisaidia kuimarisha
ushiriki wa wagombea wanawake katika uchaguzi
kwa kuwajenga uwezo wa kujinadi, kujiamini, na kushindana ili kupunguza
pengo la usawa liliopo sasa katika vyombo vya kutunga sharia.
Mapema Mratibu
Mkaazi wa umoja wa Mtaifa tananzia alilitaja tatizo la mabadiliko ya Tabia nchi
na Nishati kuwa ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili Zanzibar ambazo Umoja
huo umeamua kushirikiana na Serikali na taasisi zisizo za kiserikali kuyapatia ufumbuzi kwa haraka
kadri inavyowezekana.
No comments:
Post a Comment