SciDev.Net

Pages

Sunday, June 17, 2012


UTALII WA MISITU GHANA

Na Ali Haji Hamad, Pemba

Mapato katika Sekta ya Utalii hayaletwi na kuwa na vivutio vizuri na vingi pekee bali huletwa na ubunifu wa kuvifanya vivutio hivyo viwe vinavutia zaidi au hata visivyo vivutio basi vivutie. Hebu angalia ubunifu huu uliefanywa na Swahiba zetu wa Ghana katika msitu wao huu wa.KAKUM ulioko Kusini mwa Ghana.  Kimsingi huu msitu has nothing special to offer. Ni msitu tu kama ilivyo misitu yetu kama Ngezi au Msitu mkuu wa Micheweni .

"Bora hata Jonzani angalau kuna Vima Punju."
 Msitu wa KAKUM wenyewe una miti mirefu tu na Bonde moja liloko deep sana. Katika kuutembelea sikuwahi kuona hata karakaka sikwambii sikwambii nyoka au myama mwengine. Ila kwa ubunifu wao wameweza kuufanya msitu huu kuwa kivutio kikubwa kwa kutengeneza hiii hanging trail juu ya vilele vya miti. Ni mita kama mia saba hivi za kutembea katika hatari, woga na kiwewe lakini zinapokamilika kila mtalii anafurahi na kumuhadithia mwenzie. Ni hilo tu linalowafanya watalii wamiminike hukoo.
Sasa wa Zanzibar tunajitapa uchumi wetu unategemea utalii tumebuni nini la kuwavuta watu kutumia pesa zaidi.

Karibu KAKUM forest

Wageni wanaotembelea msitu wa KAKUM Ghana wakiwa katika hanging trail

Niliamua nami nijaribu japo kwa khofu kubwa 

No comments: