Tanzania, Zambia
zagaragazwa katika mechi za awali
Na Ali Haji Hamad
Pale kinaporoa kilemba ni muhali kwa mkuti kusalimika
Ndivyo wanavyoamini Waswahili wa Pwani. Usemi
huu ulidhihirika leo katika mechi za kuwania kufuzu kucheza kumbe la Dunia huko
Brazil mwaka 2014. Katika siku ambayo mabingwa wa Afrika Zambia imelala bao 2-0
mbele ya Waarabu wa Sudan kaika mechi ya kundi D, ilikuwa muhali kwa Tanzania
nayo kustahimili wimbi hilo kubwa na hivyo yenyewe ikajikuta ikisalima amri
mbele ya Ivory Coast kwa bao 2- 0 katika mechi ya kundi C huko Abidjan. Ushindi huu ni mwanzo mbaya kwa timu hizi
zote mbili ambazo zilionekana kupania kutaka kuvuka mabara kwenda Kusini mwa
Amerika hapo 2014.
Timu nyengine
zilizoanguka ni Congo DR mbele ya
Cameroon iliyochapwa 1-0 katika mechi za kundi H na Botswana mbele ya Afrika ya
Kati iliyogaragazwa 2-0 kwenye mechi ya kundi A. Nyengine ni Guinea ya Ikweta
iliyochapwa 3-1 na Tunisia na Liberia iliyochakazwa
kwa bao 3-1na Senegal katka mechi ya kundi J.
Sambamba na matokeo
hayo kulikuwa na matokeo ya sare ya bila kufungana katika mchezo kati ya Kenya
na Malawi kundi F na Gambia na Morroco
ziliotoka sare ya 1-1 katika mechi za kundi C. Bukinafaso na Congo nazo
ziliishia suluhu ya 0-0 kundi E.
No comments:
Post a Comment